Kutibu tatizo la moyo kwa mtoto katika hospitali ya Alkafeel

Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel mjini Karbala, limefanya upasuaji wa moyo wenye mafanikio kwa mtoto anayenyonya, hakika hospitali imekua ikipata mafanikio makubwa katika kufanya upasuaji wa watoto wadogo na wenye uzito hafifu.

Daktari bingwa wa matatizo ya moyo kwa watoto, Dokta Ahmedi Abudi amesema: Jopo la madaktari wetu limefanikiwa kumfanyia upasuaji wa moyo mtoto mwenye umri wa miezi mitatu, alikua na tatizo la uwazi kwenye moyo.

Akafafanua kuwa, kazi ya upasuaji ilidumu kwa muda wa saa nne na ilikua hatari, kwa sababu mtoto alikua anatatizo la ukuaji na alikua na uzito mdogo, akasema kuwa afya yake imeimarika baada ya ubasuari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: