Mazingira ya huzuni za kifo cha Fatuma (a.s) yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Mazingira ya huzuni yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu kufuatia kumbukumbu ya kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili.

Rais wa kitengo cha usimamizi wa haram Sayyid Khaliil Mahadi Muhammad Hanuun amekiambia kituo cha Habari kuwa “Ataba tukufu imewekwa mapambo meusi kama ishara ya huzuni za kifo cha bibi Zaharaa (a.s), aidha tutaweka mapambo meusi kwenye barabara za mji mkongwe pia”.

Akaongeza kuwa “Tayali tumekamilisha kuweka mapambo meusi na mabango yanayo onyesha dhulma aliyofanyiwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) ndani ya haram tukufu”, akasema kuwa “Uombolezaji wa msiba huu utadumu kwa muda wa siku 20, tutafanya majlisi, kutoa mihadhara na kufanya maigizo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: