Kitengo cha maadhimisho na mawakibu kimekamilisha maandalizi ya kufanya maombolezo ya huzuni za Fatwimiyya

Kitengo cha maadhimisho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimekamilisha maandalizi ya kufanya maombolezo ya kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s) katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Aqiil Yaasiriy amesema “Ratiba ya uombolezaji itaanza kwa mujibu wa riwaya ya pili (13 Jamadal-Uula) hadi (3 Jamadal-Aakhar), inavipengele vingi vyenye uhusiano na tukio hilo la kuhuzunisha”.

Akaongeza kuwa “Miongoni mwa vipengele vilivyopo kwenye ratiba ya msimu wa huzumi mwaka huu, kuonyesha hatua za Maisha ya bibi Zaharaa (a.s), na Maisha yake ya ndoa hadi alipokuja kushambuliwa katika nyumba yake, kifo chake, kuoshwa kwake, kuzikwa kwake (a.s) na mengineyo”.

Mawakibu za husseiniyya zinafunga hema katika mji wa Karbala kwa ajili ya kuomboleza msiba huo, huku kikosi cha wapiganaji cha Abbasi kikiweka picha za mashahidi wa fatwa tukufu ya kujihami kila sehemu.

Ataba mbili zimewapa kazi wanafunzi wa shule za Al-Amiid ya kuchora wanachofikiri kuhusu Maisha ya bibi Zaharaa (a.s), picha hizo zitawekwa kwenye maonyesho maalum katika uwanja wa katikati ya haram mbiti takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: