Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya inafanya warsha ya kuwajengea uwezo.. wahadhiri na mubalighina wa kike

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, inafanya warsha ya kuwajengea uwezo wahadhiri wa kike na mubalighaat kwa anuani isemayo (Tiba ya kielimu na kimwenendo).

Mkuu wa idara bibi Taghridi Tamimi amesema “Warsha imejikita katika namna ya kupambana na changamoto ambazo huwatokea baadhi ya mabinti, sambamba na kuwajengea uwezo katika mambo mbalimbali ya muhimu”.

Akaongeza kuwa “Warsha ilikua na mada tofauti zilizo wasilishwa na mhadhiri Ali Karim mtaalam wa elimu ya nafsi (saikolojia) na malezi, aidha amefafanua namna ya kutatua changamoto kielimu na kimwenendo”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Tamimi “Mihadhara iliyotolewa ipo katika mtiririko wa mihadhara ya program ya kujenga uwezo, iliyo andaliwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya anuani isemayo (Mradi wa mbeba ujumbe wa Zainabiyya)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: