Ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani imetoa tamko kuhusu ziara ya muwakilishi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa

Ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani siku ya Jumatano, imetoa tamko kuhusu ziara ya muwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Mheshimiwa Mikaeli Ankhil kwake.

Ifuatayo ni nakala ya tamko kama ilivyo andikwa kwenye mtandao wake rasmi:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Kabla ya Adhuhuri ya leo, Mheshimiwa Sayyid Sistani amempokea Mheshimiwa Mikaeli muwakilishi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa mwenye jukumu la kuweka mikakati ya kulinda maeneo ya Dini baada ya kushambuliwa katika miji tofauti duniani miaka miwili iliyopita.

Mheshimiwa amesikiliza maelezo kuhusu umuhimu wa kuishi kwa amani na kuacha vitendo vya ukatili sambamba na kuheshimu haki za watu wote.

Akaongea kuhusu matatizo wanayopata raia wa Iraq waliopo katika maeneo tofauti duniani, kutokana na kujitokeza makundi ya kidini yenye fikra za kigaidi yanayo shambulia vituo vya Dini na mali-kale za kiislamu.

Mheshimiwa akahimiza umuhimu wa kupambana na makundi hayo na kuleta uadilifu na utulivu katika jamii kama Mwenyezi Mungu mtukufu anavyo elekeza.

Mheshimiwa amepongeza kazi nzuri inayofanywa na umoja wa mataifa katika sekta hiyo, na akamtakia Mheshimiwa Mikaeli mafanikio mema katika kutekeleza majukumu yake na akampa salam za Mheshimiwa Antoniu Ghutereshi katibu mkuu wa umoja wa mataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: