Atabatu Abbasiyya inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Swidiqatu-Twahirah

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili, ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya siku ya Alkhamisi.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ukafuata mhadhara kutoka kwa Mheshimiwa Shekhe Ahmadi Rabii, akaongea kuhusu nafasi ya pande la damu ya Mtume (s.a.w.w), na mchango wake kielimu katika Dini tukufu, pamoja na kuelezea sababu iliyopelekea kifo chake (a.s).

Majlisi imehuduriwa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na ikahitimishwa kwa tenzi za kuomboleza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: