Kwa picha: watumishi wa Ataba mbili tukufu wanaomboleza kifo cha Swidiqatu-Twahirah

Baada ya Adhuhuri ya leo siku ya Alkhamisi watumishi wa Ataba mbili wamefanya matembezi ya kuomboleza kifo cha Fatuma Zahara (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili.

Matembezi hayo yameanzia katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuelekea kwenye malalo ya bwana wa Mashahidi (a.s) wakipita katikati ya uwanja wa eneo lililopo baina ya haram mbili tukufu.

Walipofika katika haram ya Husseiniyya wamepokewa na ndugu zao watumishi wa Abul-Ahraar, wakafanya majlisi ya kuomboleza Jirani na malalo ya Abu-Abdillahi Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: