Katika kumbukumbu ya kifo cha Zaharaa (a.s).. kitengo cha Dini kinafanya majlisi ya kuomboleza katika mji wa Mosul

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kinafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Zaharaa (a.s) katika mkoa wa Nainawa.

Shekhe Haidari Aaridhwi kutoka kitengo cha Dini akapanda mombari, majlisi hizo zinafanywa katika kubba kaskazini magharibi ya mkoa kwa muda wa siku tatu, nayo ni moja ya majlisi nyingi zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya katika mji wa Mosul.

Shekhe Aaridhwi ameongea kuhusu historia ya bibi Zaharaa (a.s) na nafasi yake tukufu mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume (s.a.w.w) Pamoja na nafasi yake mbele ya Ahlulbait (a.s).

Akaongea pia kuhusu utukufu wake na namna alivyo shikamana na hijabu na mafundisho ya Dini hadi katika mazingira magumu aliyokutana nayo baada ya kifo cha baba yake (s.a.w.w), kisha majlisi ikahitimishwa kwa kaswida ya kuomboleza kifo chake (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: