Kumbukumbu ya kifo chake.. matembezi ya kuomboleza msiba wa Fatuma yafanyika katika barabara za Mosul

Katika barabara ya mji wa Saadah kaskazini mashariki ya Mosul yamefanyika matembezi ya kuomboleza kifo cha Fatuma (a.s), yaliyo andaliwa na kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kama sehemu ya kuomboleza kifo cha Zaharaa (a.s).

Kiongozi wa idara ya maelekezo na msaada Shekhe Haidari Aaridhwi amesema “Matembezi yamepata muitikio mkubwa kutoka kwa wakazi wa mji huu na vitongoji Jirani, uwepo wetu umewapa nguvu wafuasi wa Ahlulbaiti wanaoishi sehemu hizi”.

Akaongeza kuwa “Wamekuja kuomboleza kifo cha mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) bibi Fatuma Zaharaa (a.s), maombolezo haya yamedumu kwa muda wa siku nne katika mji huu na miji mingine”.

Akabainisha kuwa “Watu wengi wa mji huu wamejitokeza kwenye matembezi hayo pamoja na watu kutoka vitongoji Jirani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: