Kwa kusaidia wanafunzi wa Qur’ani tukufu.. Majmaa-Ilmi imetembelea shule za Baabil

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imetembelea shule za mkoa wa Baabil.

Matembezi hayo yanasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mkoa wa Baabil chini ya Majmaa.

Safari hii wametembelea shule ya sekondari ya Alwaailiy, uongozi wa shule umepongeza sana harakati mbalimbali zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya.

Mwisho wa ziara wanafunzi wanaohifadhi Qur’ani wakapewa zawadi za tabaruku, kama sehemu ya kuwashajihisha waendelee kuhifadhi na kushiriki kwenye shughuli zinazohusu Qur’ani ambazo hufanywa na Maahadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: