Katika chuo cha Kufa.. Majmaa-Ilmi imeshiriki kwenye kongamano la kielimu

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeshiriki kwenye kongamano la kitivo cha Tarbiyya katika chuo kikuu cha Kufa, linalofanywa chini ya anuani isemayo (Vijana wa Iraq katika mtazamo wa chuo).

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa Sayyid Muhandi Almayali, amesema kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu, (ni mfano mwema katika kuendeleza vijana kwenye sekta ya Qur’ani).

Akasema kuwa, miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu inalenga kujenga vijana kwenye sekta tofauti, kupitia nadwa, makongamano, mashindano, bila kusahau mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi sambamba na semina za wanafunzi wa shule mbalimbali wakati wa majira ya joto.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: