Kumpa pole kiongozi wa waumini.. watu wa Karbala wametoka wakiwa katika maukibu ya kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha Swidiqatu-Twahirah

Watu wa Karbala wamefanya maukibu ya pamoja Kwenda kumpa pole kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib katika kumbukumbu ya kifo cha Swidiqatu-Fatuma Zaharaa (a.s).

Rais wa kitengo cha maadhimisho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Aqiil Yaasiri amesema “Maukibu ya watu wa mji wa Karbala inaomboleza kifo cha Zaharaa (a.s) katika haram ya kiongozi wa waumini (a.s) mjini Najafu”.

Akaongeza kuwa “Maukibu hii ni sehemu ya utamaduni wa watu wa Karbala, hufanywa kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na uongozi mkuu wa Atabatu Alawiyya tukufu, katika kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s)”.

Kwa mujibu wa Yaasiri, maukibu hii inaundwa na watu kutoka mawakibu tofauti na vikundi mbalimbali vya Husseiniyya katika mji wa Karbala, pamoja na waombolezaji kutoka kwenye mkoa huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: