Chuo kikuu cha Alkafeel katika mji wa Najafu kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha mtoto wa Mtume (s.a.w.w) kwa mujibu wa riwaya ya pili.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha akapanda mimbari Shekhe Swalehe Hassan Dujaili na kutoa mawaidha, mkuu wa chuo hicho na wakuu wa vitengo Pamoja na watumishi ni miongoni mwa wahudhuriaji wa majlisi hiyo.
Katika mhadhara uliotolewa na Dujaili ameeleza nafasi ya bibi Zaharaa (a.s) na utukufu wake mbele ya Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Ahlulbait watakasifu.
Kuadhimisha matukio ya kidini ni sehemu ya ratiba ya chuo kikuu cha Alkafeel, ikiwa Pamoja na matukio ya kufariki na kuzaliwa kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s).