Kitengo cha uboreshaji kinatoa mafunzo ya uokozi vitani kwa wanajeshi

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya kinatoa mafunzo ya uokozi vitani kwa wanajeshi na watumishi wa Ataba tukufu.

Mkufunzi wa uokozi vitani na utoaji wa huduma za matibabu Muhammad Aamiri amesema “Haya ni mafunzo ya sitini na sita yenye washiriki 33, ambao ni wanajeshi na watumishi wa kulinda nidham katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, mafunzo yatadumu kwa muda wa siku tano”.

Akaongeza kuwa “Ratiba ya masomo imehusisha namna ya kuokoa majeruhi wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na waliovunjika viungo”.

Washiriki wamefundishwa mbinu nyingi za kuokoa majeruhi katika ya uwanja wa vita, wamesoma kwa nadhariyya na vitendo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: