Katika mwenendo wako ewe kiongozi wangu… ratiba ya pamoja kati ya kituo cha utamaduni wa familia na idara ya wahadhiri wa kike

Kituo cha utamaduni wa familia kwa kushirikiana na idara ya wahadhiri wa kike katika Atabatu Abbasiyya wamefanya program iliyopewa jina la (katika mwenendo wako ewe kiongozi wangu).

Daktari mbobezi katika elimu ya saikolojia na tabia Shaimaa Nasoro ndio mkufunzi wa program hiyo.

Siku ya Jumapili ametoa mhadhara uliojikita kujibu swali lisemalo (Nani wewe?) akazungumza mambo mengi, ikiwa ni pamoja na maana ya mawasiliano, uhusiano wa akili na muili na sifa za akili pevu.

Program inaendelea kwa wiki ya pili, itakuwa na mihadhara 12 inayotolewa Jumapili ya kila wiki, inayo lenga kulea nafsi na kuonyesha namna ya kupambana na changamoto sambamba na kuboresha Maisha ya mtu mmoja mmoja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: