Idara ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Zaharaa (a.s)

Idara ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kupitia mfululizo wa majlisi za siku za Fatwimiyya zinazofanywa na idara hiyo.

Kiongozi wa idara bibi Adhraa Shaami amesema “Idara imefanya majlisi ya kuomboleza kwa kushirikiana na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya, majlisi hizo zimedumu kwa muda wa siku tatu, mihadhara imetaja dhulma aliyofanyiwa Zaharaa (a.s) zinazo waumiza wafuasi wa Ahlulbait (a.s)”.

Ratiba za uombolezaji imepata mwitikio mkubwa kwa mujibu wa maelezo ya Shaami, majlisi zimepambwa kwa kaswida na tenzi za kuomboleza na zilikua zinahitimishwa kwa kutoa rambirambi kwa Imamu wa zama (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: