Majmaa-Ilmi inatembelea shule za Hindiyya na kuweka mkakati wa ufundishaji wa Qur’ani kwa wanafunzi wake

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inatembelea shule zilizopo katika wilaya ya Hindiyya kwa lengo la kuanza kutoa kozi za Qur’ani kwa wanafunzi.

Mradi huo utasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Hindiyya chini ya Majmaa.

Mradi huo unalenga kuboresha kiwango cha usomaji wa Qur’ani kwa walimu na wanafunzi, kwa kuwaingiza wanafunzi kwenye kozi za usomaji wa Qur’ani pamoja na masomo mengine yanayo saidia kumjenga mwanafunzi kielimu na kimaadili.

Majmaa inamkakati mkubwa unaohusisha kufanya makongamano, nadwa na mashindano ya Qur’ani kwa lengo la kutoa elimu ya vizito viwili katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: