Filamu ya Alkhilasu.. hivi karibuni itapatikana kwenye mitandao ya kijamii

Mkuu wa kituo cha picha za katuni kutoka kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Twalibu amesema, filamu ya (Alkhilasu) itapatikana hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii iliyo chini ya Ataba tukufu.

Amekiambia kituo cha Habari kuwa “Filamu ya (Alkhalasu) inayo simulia ushujaa kwenye vita ya jihadi, na kuonyesha baba wa kiiraq aliye kwenda vitani kwa ajili ya kulinda taifa, itapatikana kwenye mitandao yote ya kijamii iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya, kila mtu ataweza kuiona”.

Akaongeza kuwa “Filamu imeandaliwa miaka miwili iliyopita na ilishiriki kwenye kongamano la sinema lililofanyika Baabil na kupata tuzo”.

Akafafanua kuwa “Lengo la kutengeneza filamu ya (Alkhilasu) ni kuonyesha japo kwa kiwango kidogo yaliyotokea baada ya kundi la kigaidi la Daeshi kuvamia Iraq, na namna raia wa Iraq walivyo jitolea kukomboa ardhi yao na kuokoa roho za wananchi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: