Katika kufuatilia utendaji.. katibu mkuu ametembelea shule za Al-Ameed

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, ametembelea shule ya Al-Ameed kitengo cha wasichana kuangalia utendaji.

Mheshimiwa katibu mkuu katika ziara hiyo amesisitiza umuhimu wa kuweka mahitaji yote ya lazima, na kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi.

Amekagua kazi zinazofanywa na idara ya shule na huduma zinazo tolewa za kielimu na kimalezi.

Ziara hii inaonyesha vipaombele vilivyo wekwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kwamba imekusudia kuona mafanikio makubwa kwenye sekta ya elimu na malezi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: