Wanafunzi wa chuo kikuu cha Al-Ameed wameweka utaratibu wa kusaidia familia za masikini wa Karbala

Wanafunzi wa kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Al-Ameed wameweka utaratibu wa kugawa misaada kwa familia za masikini zinazoishi katika vitongoji vya Karbala.

Ratiba hiyo inafanywa kwa kushirikiana na kitengo cha maelekezo ya kimalezi katika chuo.

Hakika program hiyo inafanywa sambamba na maombolezo ya kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s), wanafunzi wa udaktari waliopo mwaka wa pili wamenunua nguo na baadhi ya mahitaji ya msingi kwa ajili ya kugawa kwa familia masikini.

Lengo la program hii ni kujenga moyo wa kusaidiana na kuwafanya wanafunzi wahisi uwajibikaji katika jamii, kwa sababu kazi ya udaktari inawataka wahisi uchungu wa mtu mwingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: