Majmaa-Ilmi imetangaza kufanya semina mpya ya sauti na naghma

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza kufanya semina ya Qur’ani kuhusu sauti na naghma.

Semina hiyo inasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.

Masomo yatatolewa Jumamosi na Jumatatu kila wiki, semina itaendelea hadi watimize masomo 30 na huduma ya usafiri kwa washiriki ni bure.

Mshiriki wa semina hii anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

  • 1- Awe mkazi wa mkoa wa Najafu.
  • 2- Awe na umri wa miaka (10 – 18).
  • 3- Atume rekodi ya usomaji wake isiyozidi dakika mbili kwa njia ya mawasiliano ya kijamii.
  • 4- Aahidi kuheshimu ratiba kama ilivyo pangwa.
  • 5- Ashiriki mtihani wa majaribio utakao tolewa kwa washiriki.

Kujisajili katika semina hii tumia link ifuatayo:

https://forms.gle/fAzL2ysjj3Furo73A
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: