Chuo kikuu cha Kufa kimehitimisha nadwa ya kielimu kuhusu jukwaa la Siraaji lililotengenezwa na kituo cha teknolojia cha Alkafeel.
Msimamizi wa nadwa hiyo alikua ni kiongozi wa idara ya elimu masafa katika mkoa wa Karbala, imehudhuriwa na wakuu wa shule mbalimbali na wawakilishi wa idara za shule za serikali.
Katika nadwa hiyo vimeonyeshwa vipengele muhimu vilivyopo kwenye jukwaa hilo la kimtandao, ambalo ni sehemu ya kunufaika na teknolojia za kisasa.
Jukwaa hili lilipasishwa na wizara ya malezi na elimu na kuruhusiwa litumike mashuleni.