Kwa wanafunzi wa chuo na maahadi.. Majmaa-Ilmi inafanya nadwa ya Qur’ani

Majmaa Ilmi katika Atabatu Abbasiyya imefanya nadwa kupitia mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi awamu ya tatu ya mwaka (2022 – 2023).

Nadwa hizo zinasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.

Kiongozi wa idara ya harakati za Qur’ani katika Maahadi Sayyid Zaidi Rimahi amesema “Nadwa ya kwanza imejikita katika kuzungumzia utamaduni wa kushikamana na vizito viwili Qur’ani na kizazi kitakatifu, katika kitivo cha uchumi kwenye chuo kikuu cha Kufa, na itaendelea kufanywa kwenye vyo vikuu vyote vilivyopo katika mkoa wa Najafu”.

Akaongeza kuwa “Mradi wa Qur’ani unalenga kujenga maarifa ya Dini na kufundisha utamaduni wa kiislamu kwa wanafunzi wa vyuo”.

Kwa mujibu wa Rimahi, mradi huu unahusisha “Kutoa mafunzo ya usomaji sahihi wa Qur’ani na tajwidi, kusimamia mashindano ya Qur’ani ya tahfiidh, usomaji na kuandika, maonyesho ya picha za Qur’ani, nadwa za Qur’ani, vikao mjadala ndani ya vyuo vikuu na program ya kuendeleza walimu wa vyuo vikuu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: