Baada ya Adhuhuri ya siku ya Alkhamisi mheshimiwa Balozi wa Uturuki nchini Iraq Ali Ridha Kunai, ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu.
Amepokewa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na viongozi wengine wa Ataba.
Wamejadili njia za kusaidiana na kushirikiana kati ya Atabatu Abbasiyya na Uturuki, hususan upande wa biashara.
Katika kikao hicho Atabatu Abbasiyya imeeleza baadhi ya miradi yake na mafanikio yaliyopatikana.