Kwa ushiriki wa wageni kutoka ndani na nje ya Iraq.. Majmaa-Ilmi inafanya mahafali ya usomaji wa Qur’ani

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya mahafali ya usomaji wa Qur’ani katika Maqaam ya Imamu wa zama (a.f) ikiwa na washiriki wa kitaifa na kimataifa.

Miongoni mwa washiriki ni chama cha Qur’ani kutoka Basra na kikosi cha Misbahul-Huda kutoka Iran, mahafali hiyo imesimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.

Mahafali imeshuhudia usomaji mzuri wa Qur’ani kutoka kwa wasomaji tofauti wakiwemo wasomaji wa Atabatu Abbasiyya.

Washiriki wa mahafali hiyo wameshukuru mapokezi mazuri waliyopewa, wakasema kuwa harakati za Qur’ani zinazofanywa sehemu tofauti nchini Iraq zimesaidia sana kuinua kiwango cha usomaji wa Qur’ani hapa nchini hadi kufikia viwango vya kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: