Miongoni mwa malengo ya maendeleo endelevu.. wanafunzi wa shule za Al-Ameed wanashiriki kwa uzowefu wao wa kitaifa

Wanafunzi wa shule za Al-Ameed katika Atabatu Abbasiyya, wameshiriki kwenye kongamano la mwaka wa kwanza la kujadili malengo ya maendeleo endelevu kwa uzowefu wao wa kitaifa na wameeleza visa vya mafanikio yao katika kufanyia kazi mkakati wa (2030m).

Rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya Dokta Hassan Dakhili amesema “Tawi la Al-Ameed limeonyesha uzowefu wake ili wahudhuriaji waone utendaji mzuri kwa ajili ya kutengeneza mustakbali salama”.

Akasema kuwa “Shule za Al-Ameed zinafanya kazi nzuri ya wazi inayoshuhudiwa na kila mtu na inaendana na malengo ya maendeleo endelevu, bado zinaendelea kufanyia kazi malengo mengine ya mkakati wa maendeleo endelevu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: