Kamati inayosimamia kongamano la Imamu imefanya kikao cha kugawa majukumu

Kamati inayosimamia kongamano la wiki ya Imamu linalosimamiwa na Atabatu Abbasiyya, imefanya kikao cha kugawana majukumu.

Mjumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu Dokta Abbasi Mussawi amesema “Kikao hiki ni muendelezo wa vikao vingi tulivyo kaa siku za nyuma ambavyo tulijadili mambo mbalimbali kuhusu kongamano hilo”.

Akaongeza kuwa “Kongamano litafanywa katika msimu wa kuadhimisha Idul-Ghadiir kwa muda wa siku sata ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mussawi, kamati ya maandalizi imegawa majukumu kwa baadhi ya vitengo vya Ataba, vumuiya ya Al-Ameed na chuo kikuu cha Al-Ameed na Alkafeel, kila idara imepewa majukumu yanayo endana na shughuli zake.

Akaendelea kusema kuwa “Tunajaribu kuweka mazingira ya kielimu na kitamaduni kupitia maudhui za kongamano zitakazo eleza kuhusu Maimamu wetu watakasifu (a.s) na historia zao pamoja na athari walizo acha”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: