Kitawekwa hivi karibuni.. maelezo muhimu kuhusu kitambaa kipya cha kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maandalizi ya kuweka kitambaa kipya kwenye kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) kilicho kamilika siku chache zilizo pita, baada ya kazi kubwa iliyodumu kwa miaka mitatu katika nchi ya Misri, Lebanon, Siriya, Ufaransa na Kuwait.

Rais wa kikundi cha Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka Kuwait mbobezi wa vitambaa vya kuweka kwenye makaburi na mhisani wa kitambaa hicho Sayyid Abbasi Hashim Aalu-Bushiqah Mussawi amesema “Kazi ya kitambaa cha kwanza kilichopo kwenye kaburi la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ilifanywa mwaka 1425h sawa na mwaka 2005m, baada ya kupewa ruhusa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi”.

Akasema kuwa “Kazi ya kutengeneza kitambaa hicho ilikamilika ndani ya miaka miwili na kikawekwa kwenye sanduku la kaburi mwaka 1427h sawa na mwaka 2007m, kikawa kitambaa cha kwanza kuwekwa kwenye kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) kilicho tengenezwa kwa umaridadi mkubwa na kuwekwa nakshi nzuri”.

Akaongeza kuwa “Baada ya miaka (15) tumetengeneza tena kitambaa kipya kitakacho wekwa kwenye kaburi tukufu siku chache zijazo, baada ya kukamilika maandalizi ya kitambaa hicho”.

Mussawi akasisitiza kuwa “Kazi ilianza kwa kutengeneza kitambaa cha hariri katika nchi ya Siriya mwaka 1441h sawa na mwaka 2019m, kitambaa cha hariri kiliwekwa nakshi za majina ya Abbasi (a.s), kazi hiyo ilidumu kwa muda wa mwaka mmoja na mwezi, nyuzi zilizotumika kudarisi aya za Qur’ani ziliagizwa kutoka Ufaransa”.

Baada ya miaka mitatu ya kufanya kazi mfululizo kwa watu waliojitolea kukumikia Ahlulbait (a.s), Tumefika hatua ya mwisho ya ukamilifu wa kitambaa hiki kitakacho wekwa kwenye kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) siku chache zijazo, kwa mujibu wa maelezo ya Mussawi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: