Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha Qassim mtoto wa Imamu Kaadhim (a.s).
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha yakafuata mawaidha yaliyo gusa vitu vingi kuhusu historia ya Maisha ya Qassim mtoto wa Imamu Kaadhim (a.s).
Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi mkuu wa Idara na imepata mahudhuria makubwa.
Idara ya wahadhiri tawi la wanawake hufanya majlisi za kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) ya kumbukumbu za kuzaliwa na kufa kwao.