Aina za madini yanayopamba kitambaa kipya cha kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s)

Rais wa kamati ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka Kuwait, mbobezi wa vitambaa vya kufunika kwenye makaburi matukufu Sayyid Abbasi Hashim Aalu-Bushiga Almusawi ametaja aina za madini yaliyotumika kutengeneza kitambaa kipya kitakacho funikwa juu ya kaburi takatifu.

Mussawi amesema “Madini yaliyotumika katika kutengeneza kitambaa hiki ni Aqiiq ya Yemen, Yaquut, Zubarjad (Aquamarine), Lulu, Safaya, Satarin (Citric) na mawe ya vito tofauti”.

Akaongeza kuwa “Tumetumia kilo (5) za dhahabu halisi na kilo (8) za fedha safi, tumesimamia michoro kwa kushirikiana na mchoraji mahiri Abbasi Dhwahiri kutoka Lebanon”.

Akaendelea kusema “Kitambaa kimepambwa na michoro ya nguzo 16 ya dhahabu, zimeandikwa majina ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kila upande kuna nguzo nne na hiyo ni aina mpya ya utaalam, hali kadhalika kuna mapambo yanayo onyesha kiganja cha Abbasi (a.s) kwenye pande nne za kitambaa, kuna mapambo yaliyotiwa dhahabu na kunakshiwa vivuri kwa Duriy-Najafu upange wa kichwa na miguuni”.

Maandalizi yanaendelea ya kwenda kufunika kitambaa kipya kwenye kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) ambacho juhudi ya kukitengeneza imechukua miaka mitatu na kuhusisha nchi za Misri, Lebanon, Siriya, Ufaransa na Kuwait.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: