Kitengo cha maarifa: Tutafanya miradi miwili muhimu katika mwaka wa 2023

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeeleza sehemu ya mkakati wake wa mwaka 2023 katika sekta ya kuhuisha turathi za kiislamu na kuzitunza.

Kiongozi wa idara ya uandalizi chini ya kitengo hicho Shekhe Muhammad Dhwalimi amesema “Mwaka wa 2023m tutakamilisha kitabu cha (Waliozikwa katika Ataba takatifu) juzuu tatu, kitabu hicho kitaandika taarifa ya watu wote waliozikwa katika maeneo ya Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa “Tutakamilisha kitabu cha (Hazina za turathi) kilichoandikwa na Hassan Arabiy, kitabu hicho kinaelezea vitabu vyote vilivyo chapishwa kuanzia mwaka wa (1800m) hadi leo, kinatarajiwa kuwa na juzuu thelathini, idara inakazi nyingi ambazo zinatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka 2023m”.

Idara imeshachapisha vitabu vingi muhimu, vikiwemo vitabu vya mausua vyenye juzuu nyingi, kama vile (Mausua usulu-rijaaliyya vinne) chenye juzuu kumi, na vingine vingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: