Kuanza kwa kongamano la kielimu la nne katika chuo kikuu cha Alkafeel

Asubuhi ya leo shughuli za kongamano la kielimu awamu ya nne linalohusu fani ya udaktari na uhandisi lililo andaliwa na chuo kikuu cha Alkafeel zimeanza.

Kamati ya wahandisi na wataalam imekamilisha maandalizi yote ya kongamano hilo linalosimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Wahadhiri wa kongamano hilo wanatoka vyuo vikuu tofauti vya ndani na nje ya nchi.

Kongamano hili ni sehemu ya mkakati wa chuo unaolenga kujenga ushirikiano wa kielimu na vyuo vikuu vingine duniani sambamba na kwenda pamoja na maendeleo ya kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: