Litaendelea siku 12.. kongamano la shahada awamu ya kumi na mbili

Kongamano la shahada awamu ya kumi na mbili katika chuo kikuu cha Waasitu, limeandaliwa na taasisi mbalimbali kwa kushirikiana na Ataba tofauti ikiwemo Atabatu Abbasiyya.

Kongamano hilo linafanywa chini ya kauli mbiu isemayo “Mwenyezi Mungu anaridhia kwa ridhio lake”, kufuatia mnasaba wa kumbukumbu ya kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s).

Rais wa chuo kikuu cha Waasitu Dokta Maazin Hassani amesema, “Hakika kongamano la Shahada litafanyika kwa muda wa siku 12, litakua na vipengele mbalimbali vya kidini na kitamaduni vitakavyo fanywa kwa ushirikiano wa vyuo vikuu tofauti”.

Akaongeza kuwa, kongamano litakuwa na nadwa za asubuhi na jioni, maonyesho ya vitabu, mauwa na program za Qur’ani, kongamano litakua la kitaifa lenye zaidi ya watafiti 60 kutoka vyuo vikuu vya Iraq na vituo vya tafiti.

Shekhe Ali Saidi mmoja wa watukishi wa Atabatu Abbasiyya amesema, wahadhiri kutoka kitengo cha Habari na utamaduni cha Ataba tukufu wameshiriki kutoa mihadhara kwenye kongamano hili, wamezungumza kuhusu mambo ya Dini, Imani, na mbinu za kujenga mwanaadamu, akasema kuwa mihadhara imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi.

Kongamano litadumu kwa muda wa siku kumi na mbili, lengo kubwa la kongamano hili ni kueleza historia ya bibi Zaharaa (a.s) kwa taasisi za kisekula.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: