Kitengo cha habari na utamaduni kimefanya nadwa kuhusu ubaguzi katika bara la Afrika

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimefanya nadwa ya kielimu yenye anuani isemayo (Jangwa la afrika kusini baina ya uzowefu wa umoja na ubaguzi).

Nadwa hiyo inasimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya katika mji wa Najafu chini ya kitengo cha Habari na utamaduni.

Kiongozi wa Markazi Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Idara ya utafiti imefanya nadwa ya kujadili (Jangwa la Afrika kusini baina ya umoja na ubaguzi) wameshiriki wasomi wa kisekula kutoka chuo kikuu cha Diyala, wameeleza historia ya Afrika kisiasa na kijamii sambamba na athari yake katika jamii ya waafrika kwa mtu mmoja mmoja”.

Akaongeza kuwa “Mambo mbalimbali yamejadiliwa katika nadwa hiyo ambayo walimu na wabobezi wa mambo ya Afrika wengi wameshiriki, pamoja na familia za waafrika wanaoishi hapa Iraq na wanafunzi wa Dini kutoka Afrika wanaosoma Najafu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: