Nchini Najeria.. Kuhitimisha semina ya Aqida na Qur’ani

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimehitimisha semina ya Aqida na Qur’ani katika mji wa Sokoto nchini Naijeria.

Mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema kuwa “Leo tumehitimisha semina ya Fiqhi, Aqida na Qur’ani yenye washiriki wa umri tofauti wa jinsia zote mbili, semina hiyo ilikua inalenga kujenga uwezo wa kielimu kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika mji wa Sokoto nchini Naijeria”.

Akaongeza kuwa “Semina ilikua na mihadhara mingi, na imehudhuriwa na idadi kubwa ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s), wahadhiri wa semina hiyo walikua ni mashekhe wa nchini Naijeria, mwisho wa semina washiriki wakapewa zawadi za kuwashajihisha”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Shimri: Markazi Dirasaati Afriqiyya hufanya semina mbalimbali katika bara la Afrika, chini ya usimamizi na baraka za kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: