Kituo cha utamaduni wa familia kinaendelea na program ya (mlezi bora)

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea na vipengele vya program ya (mlezi bora) kwa wakinamama wa mji wa Karbala.

Program inavipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni kufundishwa baadhi ya kazi kama vile ushonaji, ili kuwawezesha kuwa na kipato kitakacho saidia katika maisha yao.

Hali kadhalika kuna kipengele cha kufuta ujinga, ambapo wakina mama waliochelewa kwenda shule hufundishwa kusoma na kuandika, kazi hiyo hufanywa kwa kushirikiana na kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, sambamba na mihadhara elekezi mbalimbali.

Program hii ni sehemu ya miradi inayo endeshwa na kituo cha utamaduni wa familia, inalenga wanawake kutoka familia masikini ambao wanahitaji uangalizi maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: