Kwa watumishi wapya.. kitengo cha uboreshaji kinaendelea na program ya kujenga uwezo

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya kinaendelea na program ya kuwajengea uwezo watumishi wapya.

Shekhe Muhammad Kuraitwi amesema “Mafunzo ya Dini ni moja ya sehemu muhimu katika semina hizo, watumishi hufundishwa maswala ya Fiqhi, Aqida na mambo mengine ya kidini”.

Akaongeza kuwa “Hii ni semina ya pili, na imedumu kwa muda wa siku tano, kila siku wanasoma saa tatu, watapewa mtihani ili kuangalia walichopata kwenye semina”.

Akafafanua kuwa, kuna aina tano za semina ambazo hutolewa chini ya vitengo vitano vifuatavyo: kitengo cha Dini, kitengo cha utawala, kitengo cha mali, kitengo cha mahusiano na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: