Atabatu Abbasiyya inafanya opresheni kubwa ya kusafisha malango ya Karbala

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya kazi ya kusafisha malango ya Karbala ya pande tatu.

Opresheni hii inafanywa kwa mwaka wa pili mfululizo, kwa kushirikiana na ofisi ya mkoa wa Karbala.

Makamo rais wa kitengo cha utumishi Sayyid Muhammad Harbi amesema “Watumishi wa kitengo chetu wameanza kusafisha malango ya Karbala, katika barabara ya Najafu, Bagdad na Baabil, kwa kushirikiana na ofisi ya mkoa”.

Akaongeza kuwa “Zamani tulikua tunasafisha hadi sehemu ya Haidariyya (Khaanu-Nnasu) baina ya Karbala na Najafu” akasema kuwa “Safari hii tutasafisha eneo kubwa zaidi na taasisi zote zinashiriki”.

Kazi ya usafi inafanywa ili kuufanya mji uwe na muonekano mzuri kama unavyo stahiki, ukizingatia kuwa hupokea mamilioni ya watu wanaokuja kutembelea malalo takatifu za Karbala kutoka kila sehemu ya dunia, akasisitiza kuwa “Usafi ni jukumu la kila mtu, sehemu za malango ya kuingia Karbala zinawakilisha picha ya mji, hivyo yapasa ziwe safi, na jambo hilo ndio tunalofanya kupitia opresheni hii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: