Majmaa-Ilmi inaendelea kufanya vikao darasa kuhusu Qur’ani.. kwa wanafunzi wa bweni

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya Inafanya vikao darasa vya Qur’ani, kupitia mradi maalum wa mwaka (2022 – 2023) wa Qur’ani kwa wanafunzi wa bweni katika mkoa wa Najafu.

Vikao hivyo vinasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.

Kiongozi wa idara ya harakati za Qur’ani katika Maahadi Sayyid Zaid Rimahi amesema kuwa “Vikao darasa vinafanywa kwa wanafunzi wa bweni, vinalenga kuwajengea uwelewa wa mwenendo wa vizito viwili Qur’ani na kizazi kitakasifu”.

Akaongeza kuwa “Kikao darasa cha nne kimefanywa kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Kufa, wanafunzi wa chuo hicho wamehudhuria kwa wingi”, akasema kuwa “Vikao darasa vinaendelea na vinahusisha vyuo vyote vilivyopo katika mkoa wa Najafu”.

Akaendelea kusema “Mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo na Maahadi unahusisha kufanya semina za usomaji sahihi wa Qur’ani na kanuni za tajwidi, mashindano ya kuhifadhi Qur’ani na mengineyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: