Kuadhimisha siku ya bwana wa lugha.. Jumuiya ya Al-Ameed imefanya nadwa ya kielmu

Jumuiya ya Al-Ameed imefanya nadwa ya kielimu chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya lugha ya kiarabu chini ya anuani isemayo “Lugha yetu ya kiarabu ni bwana wa lugha”.

Kwenye nadwa hiyo mada za kitafiti zimewasilishwa chini ya usimamizi wa Dokta Sarhani Jafaat Salmaan, miongoni mwa mada zilizo wasilishwa ni: uhusiano wa kuhifadhi Qur’ani na lugha ya kiarabu, iliyowasilishwa na Dokta Swalehe Shimri, changamoto zinazoikumba lugha ya kiarabu, imewasilishwa na Dokta Abdulkadhim Muhsin Yaasiri, lugha ya kiarabu ni bwana wa lugha, imewasilishwa na Dokta Iswaam Kaadim Alghalibi, lugha ya kiarabu na uhusiano wake na mfumo wa dunia, utafiti katika mpangilio wa lugha, imewasilishwa na Dokta Ali Jaasib Abdullah, upekee wa lugha ya kiarabu ukilinganisha na lugha zingine, imewasilishwa na Dokta Muayyad Abdulmuni’im Shamisawi, viwango vya miujiza ya lugha katika Qur’ani tukufu, imewasilishwa na Dokta Majidi Najariyani.

Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya lugha ya kiarabu yamepambwa na mashairi kutoka kwa washairi tofauti waliosoma beti kuhusu lugha ya Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: