Kituo cha utamaduni wa familia kimepokea wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Karbala

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimepokea wanafunzi kutoka kitivo cha utawala na uchumi katika chuo kikuu cha Karbala, kupitia program yake ya utamaduni ya (kujenga uwezo).

Program imefanywa katika ukumbi wa shamba la kunazi ilikua na vipengele vingi, ukiwemo mhadhara wenye anuani isemayo (Hatua za kuelekea kwenye mafanikio) uliotolewa na Adhraa Ahmadi, na kipengele cha (Kutoka kwenu hadi kwenu) ambacho ni kipengele cha maswali na majibu, kipengele cha (Picha na maelezo) kilichokua na waongozaji wawili Nabaa Swabahi na Imaan Auni.

Program imehusisha mashindano ya utamaduni na kidini, inalenga kujenga wanafunzi waweze kukabliana na mazingira ya usomaji.

Kituo kinaendeleza program zilizo andaliwa kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo, kwa lengo la kujenga uwelewa wa utamaduni na Dini sambamba na kuelekeza mwenendo wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: