Kitengo cha habari na utamaduni kinashiriki kwenye maonyesho ya vitabu katika kongamano la Shahada kikiwa na zaidi ya aina 200 za vitabu

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimeshiriki kwenye maonyesho ya vitabu yanayofanyika katika chuo kikuu cha Waasit kikiwa na zaidi ya aina 200.

Kiongozi wa idara ya maonyesho Sayyid Muhammad Aaraji amesema “Kitengo cha Habari na utamaduni kimeshiriki kwenye maonyesho ya vitabu kikiwa na zaidi ya aina 200 za vitabu”.

Akaongeza kuwa “Tawi la Atabatu Abbasiyya limekua na upekee kwenye maonyesho hayo, watu wanamiminika kwa wingi kwenye tawi hilo kuangalia vitabu, kununua na kuuliza maswali yanayohusu Ataba tukufu”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Aaraji, kitengo cha Habari na utamaduni kinavitabu tofauti, kama vile vitabu vya historia, dini na utamaduni vinavyo lenga kueneza maadili mema kwa vijana na jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: