Kuhusu vipaji vya vijana.. nadwa ya kitamaduni katika mkoa wa Bagdad

Kitengo cha Habari na utamaduni kimefanya nadwa yenye anuani isemayo (Vijana kuhusu matumaini na ndoto zisizo na maana) katika mkoa wa Bagdad.

Nadwa hiyo inasimamiwa na kituo cha tafiti za kielimu kwa kushirikiana na jumuiya ya Al-Ameed.

Mkufunzi wa nadwa Shekhe Hassan Jawadi amesema “Vijana wanachangamoto kubwa za kitamaduni na kielimu, changamoto hizo huwarudisha nyuma”.

Akaongeza kuwa “Lengo la kufanya nadwa ni kuelekeza njia sahihi ya kuweka malengo mazuri, ili kuwaepusha kuwa na ndoto zisizo fikika katika Maisha yao”.

Jawadi akafahamisha kuwa “Hii ni miongoni mwa nadwa ambazo hufanywa kwa kushirikiana kati ya kituo cha tafiti za kielimu na jumuiyya ya Al-Ameed katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Nadwa hiyo ambayo imefanywa katika Husseiniyya ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwenye kitongoji cha Biyaau, imehudhuriwa na vijana wengi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: