Majmaa-Ilmi imefungua uwanja mpya wa elimu na Daaru-Makhtutwaat ya Iraq

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya kupitia kituo cha uchapishaji wa msahafu mtukufu, imefungua uwanja mpya wa elimu kwa kushirikiana na Daaru-Makhtutwaat ya Iraq jijini Bagdad.

Yamesemwa hayo baada ya ziara ya Mheshimiwa Shekhe Dhiyaau-Dini Zubaidi mkuu wa kituo cha uchapishaji wa msahafu kwa Daaru-Makhtutwaat ya Iraq jijini Bagdad alipokutana na Dokta Ahmadi Karim Alyawi, wakaongea kuhusu nakala-kale za Qur’ani zinazomilikiwa na Daaru-Faharasi, ambazo ni nyingi na muhimu.

Mkuu wa Daaru-Makhtutwaat za Iraq, Dokta Ahmadi Karim Alyawi amepongeza Atabatu Abbasiyya tukufu kwa namna inavyo saidia sekta ya nakala-kale na faharasi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: