Kilimo cha umwagiliaji.. mafanikio mapya katika shirika la Khairul-Juud

Shirika la Khairul-Juud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, limefanikiwa kwenye kilimo cha umwagiliaji kwa kustawisha mimea kwenye ardhi ambayo sio nzuri kwa kilimo.

Mkuu wa mauzo na masoko wa shirika hilo, Mhandisi Falahu Alfatli amesema “Shirika letu limefanikiwa kwenye kilimo cha umwagiliaji wa kutumia maji ya visima na teknolojia za kisasa”.

Akaongeza kuwa “Kupitia teknolojia za kisasa tumeweza kuleta mapinduzi makubwa kwenye kilimo cha Iraq, sambamba na matumizi ya pembejeo za kienyezi zisizokua na kemikali zenye madhara kwa binaadamu na mazingira”.

Miongoni mwa faida za kilimo cha umwagiliaji ni “Kinawezesha kulima kwenye ardhi ambayo sio nzuri kwa kilimo na mimea yake huwa misafi na mizuri kwa matumizi ya binaadamu, haina madhara yeyote kwa watu na mazingira kutokana na aina ya pembejeo tunazotumia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: