Kitengo cha Dini kinafanya semina ya kifiqihi kwa wapiganaji wa kikosi cha ulinzi wa haram mbili tukufu

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya semina ya masomo ya fiqihi na Aqida kwa wapiganaji wa kikosi cha ulinzi wa haram mbili tukufu.

Makamo rais wa kitengo hicho Shekhe Aadil Muhammad Wakili amesema “Kitengo cha Dini kinafundisha Fiqihi na Aqida kwa watumishi wa Ataba tukufu hususan Atabatu Abbasiyya kwa lengo la kusambaza masomo ya Dini na mafundisho ya madhehebu ya Ahlulbait (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Tunaona ni jambo la muhimu kufundisha maswala ya Fiqhi na Aqida kwa watumishi wa Ataba na mazuwaru watukufu, hivyo tumeona tutoe mafunzo haya kwa walinzi wa haram mbili tukufu”.

Mmoja wa wapiganaji amesema “Semina ilikua nzuri na yenye mafanikio makubwa, kupitia semina hii tumetambua umuhimu wa kushikamana na bwana wa mashahidi (a.s) na kuhudumia mazuwaru wake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: