Maahadi ya Qur’ani tukufu imefanya warsha ya kuwajengea uwezo watumishi wake

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefanya warsha ya kuwajengea uwezo watumishi wake.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema “Maahadi inafanya nadwa na warsha za kuwajengea uwezo watumishi wake, kupitia walimu wa kitengo cha malezi na elimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa “Warsha imeanza kwa kuangalia mkakati wa utawala bora chini ya muongozo wa mkufunzi Imaad Dhwalimi, zikafuata mada zingine tofauti, kila siku imejadiliwa mada moja kwa muda wa siku tatu”.

Warsha inahusisha watumishi wote wa Maahadi pamoja na wale wa Raudhat-Ahbaabul Kafeel chini ya Maahadi, kupitia mradi wa kuwajengea uwezo watumishi na kuwafanya waendane na maendeleo ya sasa, kwa mujibu wa maongezi ya Aljaburi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: