Majmaa-Ilmi imetangaza shindano la kutengenezo nembo ya moja ya kituo chake

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza shindano la kutengeneza nembo ya kituo chake cha kuchapisha Qur’ani.

Mshindi wa shindano hilo atapewa zawadi ya dinari (500) za Iraq, kwa masharti yafuatayo:

  • 1- Iwe inaeleweka kwa urahisi.
  • 2- Iwe na alama ya msahafu na Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • 3- Iwe na rangi ya kijani iliyoiva.
  • 4- Siku ya mwisho ya kupokea kazi hizo ni Jumanne ya tarehe (10/1/2023m).
  • 5- Majmaa inahaki ya kupendekeza marekebisho kwenye nembo itakayoshinda kwa kushauriana na mtengenezaji wa nembo husika.
  • 6- Nembo zitumwe kwenye telegram kupitia namba ya simu ifuatayo (0785128865).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: