Kuhitimisha program ya wiki hii kwa watumishi

Kamati ya mikakati katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imekamilisha program ya mafunzo ya wiki moja kwa watumishi wapya.

Program hiyo imesimamiwa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kujenga uwelewa wa masomo ya Dini na utamaduni pamoja na kujenga ukaribu baina ya watumishi.

Program inahusisha masomo tofauti, mashindano na kutembelea sehemu mbalimbali.

Program hudumu kwa muda wa siku tano kwa kila kundi, ili kuhakikisha watumishi wote wanashiriki kwenye program hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: