Ujumbe kutoka kitengo cha Dini umetembelea vikosi vya wapiganaji wa Hashdu-Shaabi katika mkoa wa Diyala

Ujumbe kutoka kitengo cha Dini chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, umetembelea vikosi vya wapiganaji wa Hashdu-Shaabi kwenye kitongoji cha Naftu-Khana katika mkoa wa Diyala.

Idara ya maelekezo na msaada imetoa zawadi kwa wapiganaji hao, kama sehemu ya kutekeleza maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.

Shekhe Haidari Aaridhwi kutoka kitengo cha Dini amesema “Hii ni moja ya ziara nyingi tunazofanya kwa vikosi vya wapiganaji vya Hashdu-Shaabi kwenye miji tofauti hapa Iraq”.

Akaongeza kuwa “Lengo la ziara hii ni kuwatia moyo na kuwapa zawadi wapiganaji, sambamba na kuwapa mawaidha kuhusu jihadi na kulinda taifa”.

Kwa mujibu wa Aaridhwi, Atabatu Abbasiyya tukufu inatilia umuhimu mkubwa swala la kutembelea wapiganaji waliopo kwenye uwanja wa mapambano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: